KIJANA WA MAANA:
Sehemu ya kwanza……………………………
Kijana kuwa wa maana hiyo ndio kiu ya watu
waliokatika rika hili na ndo maana wanatumia wakati wao mwingi kujishughulisha
ili mwisho wa siku wawe wa maana katika nyanja zote za kimaisha, na pindi
anaposhindwa kutimiza hazma hii uwa moyo wake unakuwa mnyonge sana na hatimae
uweza kufikia maamuzi ambayo yanaweza hatarisha maisha yake kwa kiasi kikubwa
sana baadhi yao uweza kujiingiza katika madawa ya kulevya, vitendo vya ngono na
matendo ambayo yanayo hatarisha maisha yao na hata kuvunja sheria za nchi.
Kwa uhakika kijana ni hatua ambayo inaaminika ni hatua ya mabadiliko,
kwahiyo ni hatua ambayo unahitaji uangalifu mkubwa katika kufanya maamuzi
sahihi.
Kuna mifano mingi ya watu ambao walio fanikiwa
lakini wamejenga misingi mizuri tangu ujana wao na hatimae kuja kuvuna yale
ambayo hatua inayofuata.
Kutokana na maelezo ya hapo awali tutakwenda
kujifunza hatua kwa hatua kuhusu kijana na hatimae tumpate kijana wa maana.
Napenda kuzungumzia mapema sana tunapozungumzia
kijana wa maana hatuzungumzii muonekano mzuri(physical appearance) au kuvaa
mavazi ya gharama sana.
UJANA
ni hatua ya tatu(biology) ambayo kila mwanadamu anapitia ili kufikia hatua ya
uzee(utu uzima). Ni hatua mbayo watu ambao wanapata neema kufikia huwa
wanapenda kudumu katika hatua hii pasipo kutaka kwenda hatua ya uzee.
Mithali 20:29@
Kama kipindi ambacho unaweza kuifaidi dunia kwa
namna ya kipekee ni hatua hii kwani unakuwa unaweza kufanya mengi na ukakizi
haja yako na kutokana na uwezo wako katika uchumi au uimara wa mwili wako.
Hii nafasi ambao haijurudii jambo ambalo ulitakiwa
kulifanya kipindi usitegemee kulifanya katika hatua nyingine kwakua kila hatua
kuna mambo yake.
Tutakwenda
kuangalia mambo mbalimbali ambayo yanaweza fanya ujana kuharibika;
I.wapi umezaliwa? Makuzi(kulelewa)
gani umepitia?
II.maisha gani
umepitia?
III.uhuru
uliopewa na maamuzi uliyofanya.
I.(a)wapi umezaliwa?
Kila mwanadamu anachimbuko lake japo anaweza kulijua
au kutolijua kutokana sababu mbalimbali ila kubwa sana lakutambua vile chimbuko
lilivyo ndivyo ulivyo, kwakua wewe ulivyo unawakilisha chimbuko lako na kamwe
hauwezi kuwakilisha chimbuko ambalo si lako hivyo njia nzuri ya kutoka mahali
ni vizuri wapi umezaliwa kwakua mahali ulipo zaliwa panajenga msingi katika
maisha yako unategemea ukawa mzuri au ukawa mbaya, ni wazi ubora mti utegemea
shina lilivyo na sio matawi wala jambo jingine.
Kila jamii husika ina namna ya kumchukulia mtoto au
kijana kutokana na misingi ya jamii husika na sio kama jamii nyingine.
Namna wanavyo mpokea mtoto unajengwa na mtazamo wao
wakufanya jambo hilo ambao unaweza kuwa umejengwa na misingi ya kikabila katika
mila na desturi.
Hakuna kabila ususa afrika yetu inayo mpokea
mtoto katika misingi ya kumjua Mungu na
kumfanya ampende Mungu maisha yake yote, bali watu ufikiria namna ya kumfanya
hayafurahie maisha yake hapa duniani pasipo kuhofia maisha yaliyopo baada ya
kutoweka duniani.
Mwanzo 6:5
II wafalme 21:1-12
II wafalme 22:24-26
Maisha ya wazazi yametawaliwa na hofu kuhusu hatma
ya watoto wao kwani matazamio ya wazazi hawa ni kuona ustawi wao wangalipo
duniani na hata wa kizeeka wapatwe kutunzwa hivyo uwabidisha katika kuwafanya
wawe na mwelekeo ulio bora wa maisha yao hapa duniani hili silo tatizo kwa kua
mafanikio ya mtoto ndio furaha ya mzazi na kushindwa kwa mtoto ndio aibu kwa
wazazi.
Pamoja na hayo yote ni vizuri kutambua kwa mtoto
wako ili aweze kuishi vyema hapa duniani ni muhimu sana aweze kuishi huku
akimjua Mungu muumba dunia na elimu katika kupanua ufahamu haifahamu dunia
katika namna ya kibinadamu.
Pale ulipo zaliwa panaweka nuru au giza katika
maisha yako ya baadae kwa hiyo shina lina hamua uishi vipi hapa duniani katika
hali njema au ya mateso.
Ayubu 14:4
Kutoka 20:5
Waebrania 7:9-10
Yale maneno unayoambiwa tangu mtoto yanajenga vitu
katika maisha ambayo athari zake utaanza kuziona mara baada tu ya kuanza
kutawala maisha yako. Mathalani watoto wa kipalestina wanaopandikizwa chuki
dhidi ya waisraeli hayo maneno yanakuwa na nguvu na kusimama kutoa mwelekeo wa
maisha yako.
Usipopata msaada utaangamia na usipo kuabali kupokea
huo msaada bado utaangamia.
Prepared by ;
Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
Asante tukutane wakati wakati ujao…………………..!!!!!!!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni