Jumatano, 4 Desemba 2013

VIGEZO VYA KUPENDWA NA MUNGU



VIGEZO  VYA  KUMPENDA  MUNGU (UTHIBITISHO)

Hili ni jambo la kawaida sana kwa mtu yeyote mtu utakaye mpenda lazima awe na sifa ambazo wewe unazozitaka na wala haiwezi kutokea wewe hali ya kupenda penda hovyohovyo mtu asipite mbele zako.

Mungu apendwi kwa kuwa umejisikia kumpenda au umeona tu ipo haja ya kumpenda kwa wakati Fulani,bali viko vitu ambavyo Mungu akiviona anajua tu wewe sasa umeamua kumpenda kwa dhati sio unajaribu kumpenda.Katika kitu kizuri Mungu hashawishiki kwa maneno ya kawaida tu bali moyo unao jua unachofanya ndio unao mtisha Mungu.

Sio kwa vigezo vyako ndio ukaweze kumshawishi Mungu akupende bali ni kwa vigezo vyake, ikiwa kwa ni kwa vigezo vyako basi utajipenda mwenyewe na kama kwa vigezo vyake basi yeye atakupenda.

i.maisha ya kuacha vyote kwa ajili ya kristo kwa ukamilifu

unapoamua kumfuata yesu uyashikilie hayo maamuzi ulio yachukua na moyo wako ukushuhudie pasipo shaka ndani yako.

Ni jambo la muhimu kwa watu wanao amua kupendana ili waweze kuzidi na kushamili lazima asiwepo mtu mwingine akawa na nafasi sawa ndani yenu kama mlivyo.

Hali ya kuacha vyote haimaanishi kwamba uache kusoma kama unasoma,kuacha kazi kama unafanya kazi  au una fanya shughuli yeyote ya halali ukaiacha sivyo.

Bali ni vile moyo wako unavyo yapa kipaumbele/uzito mambo ambayo yanamfanya Mungu kuzidi ndani ya maisha yako.

Tamani sana maisha yako yawe na muunganiko wa kweli na Mungu yenye utiisho,mamlaka na nguvu pamoja na ushindi.

Tamani kuona maisha yako yakimuonyesha Mungu katika mwenendo mzima ulionao watu waone huruma,upendo,uponyaji,uweza wa Mungu penda kuona Mungu akiyafurahia maisha yako kuliko mtu yeyote hata mpenzi wako.

Mathayo 16:24-25

Kubali yote ya kukute lakini kamwe yasivuruge Mungu katika maisha yako yakaleta utengano wako na Mungu.

Yohana 16:27


ii.maisha ya kuangalia Mungu anakuonaje na wala sio wanakuonaje?

Siku zote motto mwenye akili uangalia wazazi wake wapendacho na si majirani wanachosema kwakua utambua furaha ya wazazi ndio furaha yake.

Mithali 10:1

siku zote watu wanakuona vile unavyoonekana hawa wezi kukuongeza au kukupunguza bali nafasi yao ni kusema katika hali ya kukosoa au kupongeza kulingana na mtazamo wake.

Una haja ya kuogopa hao bali unao nafasi ya kuwasikiliza na kuwa heshimu lakini mmbo mengine yote yana baki ndani yako binafsi kwani wewe ndio unajipenda hasa kuliko mwingine.

Maisha yasiyo ambatana na hofu ya kibinadamu bali ni hofu ya Mungu iliyo katika hali ya kupenda tena kwa furaha.

Maana Mungu katika wengi anakuangalia wewe binafsi hivyo katika wengi muangalie yeye binafsi.

Mhubiri 7:26(b)
Luka 12:22-24

iii.maisha yasiyo tazama aibu ya sasa bali aibu ya baadae(aibu ya milele)

Ishi maisha ya kutopata aibu ya milele kuliko aibu ya sasa isiyo dumu, hatima ya wanadamu iko mikononi mwa MUNGU.

Mathayo 10:32-33
Luka 12:20-21

Hakuna kisichikuwa na mwisho katika ulimwengu huu bali ni NENO  LITOKANALO KINYWANI  MWA  MUNGU.

Ishi isha ambayo kishindo cha mbingu kitaitikia na kukukubali na kusema kweli wewe ni mtu uliye amua kumpenda Mungu.

iv.maisha ya kufungwa nira ya kristo

haya ni maisha ya kumjua zaidi kristo kuliko chochote kwa kuwa ndicho kilichopewa nafasi kubwa ndani ya moyo mwake.

Unaposikia kitu kinachoitwa Mungu moyo wako unashtuka haoni nafasi ya kutulia kwa kuwa hauoni jambo ambalo litazuia kitu chochote kitazuia upendo wako kwake.

Moyo wako hutamani/haupendi kuona akisijisikia vibaya kwa ajili yako wewe unatamani kuona siku zote anakuwa na furaha pindi anapoona uwepo wako.(wewe ndio furaha yake)

Matendo 15:26
Mathayo 11:28-30

Utayari wako uwe kwaajili ya Mungu tu kwa ukamilifu wote mtumikie bwana wako pasipo shaka yoyote tena katika hali ya furaha isiyokoma.

Matendo 21:13

v.maisha ya kujenga mwili wa kristo

Na wala sio maisha yanayowaza kwa ajili yake binafsi bali ni mawazo yaliyojaa nimfanyie nini Mungu leo kizuri kuliko jana, hii ni hali muhimu sana kwa watu wanaopendana uwa wanawaza kwa ubora siku kwa siku unaongezeka.

Unatamani kuona furaha yake ikizidi siku hadi siku na sio ipungue ili linakuwa ni jukumu lako kwa kuwa UNAMPENDA.

Huu ndio moyo ambao Mungu anautafuta ambao utasimamisha ufalme wake na kuimalika na kuwa wakumu usio tikisika milele.

Mathayo 16:18
Waefeso 4:11-12

Unajenga mwili wa kristo kwa njia ya PENDO LA MUNGU NDANI YAKO.

Imeandaliwa na ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com

KILA LA KHERI…………..RAFIKI


Alhamisi, 3 Oktoba 2013

KIJANA WA MAANA YUKOJE?



KIJANA WA MAANA:

Katika kuendelea juu ya kuwa kijana wa maana mbali na kuwa na pesa tu na vitu vingi vinaonekana vya thamani kwa mwanadamu.tunapenda tena tuangalie katika kipengele kinachofuata.

iii.uhuru na uamuzi uliochukua

kila familia ina namna ya kuchukulia au kulea watu wake katika jamii hiyo kuna watu waliokuwa na uhuru na wengine waliokosa uhuru na wote kuna maamuzi waliochukua na hatimae wakawa jinsi walivyo.

Hakuna jambo ambalo linakaa katika moyo wako kwa muda mrefu kama maamuzi uliochukua halafu ukawekwa katika hali mbaya, kwakua katika mazingira haya hakuna wa kulaumiwa ila ni wewe binafsi.

Haijalishi ni shindikizo gani lilikusukuma hatimae ukaamua maamuzi uliyo yachukua bali kitakachoangaliwa hapo ni matokeo uliyo yachukua.

Yako maamuzi uliochukua pasipo kujua kwa usahihi wa jambo husika na kuna maamuzi uliochukua kwakua uliona ni sahihi kwa wakati ule lakini mwisho ukaujeruhi moyo wako.

Ezekieli 16:15-16,22-26

Unaweza ulipewa uhuru mkubwa nyumbani kwenu kwa lengo la wazazi kutaka uyafurahie maisha yako na uwafurahie wazazi wako lakini ukautumia ule uhuru katika maslahi yako pasipo kuangalia usahihi wa kitu naam kasha ukaona matokeo yake.

Kumbuka kwamba jambo ukisha lifanya linabaki kuwa historia katika maisha yako na wala haifutiki bali inabaki kuwa kumbukumbu ambayo inaweza kuwa na nguvu ndani ya maisha yako au isiwe na nguvu yote inakutegemea wewe binafsi.

Kunawezekana ulikuwa unakataa kutokana na mafundisho mazuri uliyofundishwa na wazazi wako nay ale uliyojifunza ukayafanya kuwa ni maisha yako lakini kutokana na maneno ya mtu akakushawishi hatimae 
ukaamua kukubaliana nae na hatimae ukaona matokeo yake yanaweza kuwa mabaya au mazuri inategemea na jambao lenyewe.

Mathayo 7:10-23

Yamkini hapo awali ulikuwa mtu mzuri sana hata wewe binafsi ulijitamani lakini ukakutana na rafiki mbaye kwa kiasi kikubwa alibadilisha maisha yako na kuwa kwa namna ya yeye ambayo ataifurahia (kutumia madawa ya kulevya(bangi,unga n.k), kujichua nawe ukakubaliana na njia hizo kumbe unajiharibu kisakolojia(akili).hata Mungu afurahi lakini kwa uhuru uliopewa ukaingia pengine hata bila ya kuruhusiwa hatimae matokeo ukayaona.

II petro 2:14-15

Waefeso 5:11-12


HAKUNA RAFIKI ATAKAYE  KUPENDA KATIKA HALI YOTE,
(pendo la weza kupungua hatimae kupotea kabisa. Yesu ndiye rafiki)


Yamuhimu:

I.rudi kwa Mungu(wokovu)

Mungu anakupenda vile ulivyo kwakua yeye ndie chimbuko la wanadamu lakini pindi utakapo okoka kwa Mungu unakuwa na kibali kwa Mungu cha tofauti.

Hata kama umepoteza mwelekeo jua kwamba ndani ya Mungu kuna mwelekeo sahihi ambayo ukimwamini basi utapata mwelekeo sahihi.

Mungu si kama wanadamu yeye afikiri kuhukumu bali ufikiria namna gani ya kukutoa mahali ulipo na kwenda mahala pengine penye ubora wako katika maisha yako.

II nyakati 33:1-3,11-13

Ona ni kweli ulikuwa unamtenda Mungu dhambi ya wazi au ya silini kiri kuwa wewe ndiye ambaye ulimkosea Mungu na sasa umeamua kurudi kwa moyo wote pasipo kuangalia kushoto wala kulia.

Mitahali 28:13

Onyesha ya kwamba unamwitaji Mungu kuliko chochote kwakua ni ndani yake tu ndiko kuliko na usalama na sio mahala pengine na ukijua lile alilopanga Mungu ndilo litakalo timia na sio alilopanga mpenzi wako wala wewe binafsi kwa hiyo Mungu kiwa upande wako kila kitu kitakuwa sawa.

Onyesha hali ya kumwitaji Mungu kwakua yeye anaweza kubadilisha leo ikawa kesho na kesho ikawa leo hivyo anauwezo wa kubadilisha historia yako akakupa historia nyingine iliyo bora zaidi ya vile unavyofikiria.
Tambua ulitumia mwili wako visivyo na wakati wako lakini sasa umeamua kutoa mwili wako kwa ajili ya Mungu peke yake.

I wakorintho 6:19

II wakorintho 7:9-10



Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com




“Itakuwa vizuru tukikutana tena katika wakati mwingine………..BARIKIWA



Jumatatu, 16 Septemba 2013

KIJANA WA MAANA YU KOJE?



KIJANA WA MAANA:

Katika kuendelea juu ya kuwa kijana wa maana mbali na kuwa na pesa tu na vitu vingi vinaonekana vya thamani kwa mwanadamu.tunapenda tena tuangalie katika kipengele kinachofuata.
                                          

                                              II.Maisha uliyopitia (mateso & shida)

Maisha ni mchangunuo wa mambo mbalimbali ambayo mwanadamu anapitia tena katika hali tofautitofauti ambayo mwanadamu anapitia kila maisha mtu binafsi aliyopitia uacha alama ndani ya moyo wako na kuwa ni elimu kwa mtu husika au uzoefu alioupata katika maisha yake.

Katika sayari ya dunia tuliyonayo sasa wapo watu amabao wanaishi maisha tofautitofauti katika hali nzuri/njema na hali mbaya/duni.pia wako watu walianzia hali njema baadae wakaishia pabaya na wengine wapo walioanzia katika hali mbaya baadae wakaishia katika hali nzuri/njema na wengine wamekuwa na mchanganyiko na hatimae wakaishia katika hali iliyo njema au iliyo mbaya, inategemea na familia uliyotoka pamoja na hayo pia kuna kundi la watu ambao maisha yao ni maumivu mwanzo mwisho.

Na maisha uliyoyapitia ndio leo uko vile ulivyo katika muonekano ulionao sasa wa huzuni au wa furaha.
Hakuna maisha ambayo uliyo yapitia mbali na wokovu yakawa na kibali kwa Mungu kwa namna yoyote haijalishi jamii inakukubali au haikukubali katika muonekano wowote wa dunia hii hauna kibali kwa Mungu bali ni vile Mungu anavyotaka tu ndivyo utaupendeza moyo wa Mungu.

Unapoishi maisha mbali na wokovu unakuwa unajifunza vitu vingi na kushiriki mambo ambayo yanawezekana kuonekana katika ubora wake katika jamii yako jua jambo lolote unalojifunza au kushiriki lina jenga mambo ambayo yataendesha maisha yako katika namna unavyoelewa.

Na pindi usipokuwa makini unaweza kujikuta katika hali tete ambayo itakusumbua katika maisha yako inaweza kuwa kikwazo kati yako na Mungu kwa kiasi kikubwa na yanaweza kuwa kikwazo kikubwa katika kuleta maendeleo yako katika maisha ya rohoni na ya mwilini.


Kama binadamu wakawaida kuna yako mambo uliyokuwa unayafanya unapokuwa pekee yako chumbani au mahali popote pa siri(kufanya mapenzi, kujichua, mawazo ya ukatiri na dhana ya kutaka kujiua)


I wathesalonike 4:3-5

Kuna muonekano ambao Mungu alikusudia katika kutimiza hazma yake katika kukuleta hapa dunia kuna namna ya wewe kuwa usiwe tu kiolela. Kama baba aliye makini anavyoweza kumwandalia mwanawe hatma njema ya baadae.

Luka 12:2-3

Muonekana wako wa awali unaonekana sasa kwa kuwa vile utakavyo ishi itategemea sana vile unavyoelewa na kukubaliana na hali uliyokuwa nayo hapo awali.

II Samweli 12:12

I Wakoritho 6:13-20

Mwanzo 8:21

Mambo yoyote yanapokuwa yakiendelea katika nafsi ya mtu husika na wakati wingine mtu huyu uweza kutekeleza yale yanayoendelea ndani yake.

Na pindi unapojaribu kutenda jambo hili kuna mambo yanazaliwa kutokana na tendo hilo ambayo yanakuwa na muonekano mbalimbali:

Hesabu 31:17-18
                   
                    i)kuna hali ya kushutuka pindi mambo hayo yanapotamkwa.
  
 ii) hofu na kutojiamini utawala na kuwa na nafasi katika maisha ya muhusika.
           
 iii) hali ya wasiwasi na mashaka juu ya magonjwa ya zinaa mathalani. Ukimwi ,kisonono na mengine mengi.
          
 iv) wengine wana kuwa na hali ya ukimya na wengine inawatokea hali ya kupenda kuongea pasipo sababu.
         
 v) kuchukia haina ya jinsia inaweza kuwa ya kike au ya kiume.
          
vi) mawazo sugu ambayo yamekosa muafaka.
         
vii) kutoa mimba( lina hasara kubwa katika maisha ya mtu husika)

Ni vizuri kutafakari wapi umetoka na je! Unaenda wapi na je! Utafika je, hiyo safari yako uwezekano wa kufika upo kwa kiasi gani na uko tayari katika chngamoto mbalimbali katika kufikisha ile hatma yako.

Ni vizuri kutambua kuwa unahitaji neema ya Mungu katika kukufikisha pale ambapo yeye mwenyewe amepanga na kukusudia ya kuwa wewe upate kufika mahali husika na sio pale ambapo unatamani wewe tu.

Hii iko wazi ujana ili uweze kuwa mzuri au mbaya unategemea sana nani ni kiongozi wako katika kuongoza maisha yako.

Yohana 10:10
Mbali na Mungu hakuna ujana ulio salama kama ujampa yesu maisha yako kwa ukamilifu wake hauwezi ukawa salama.

Isaya 40:28-31
Hakuna mtu anajua jinsi unavyotakiwa kuwa isipokuwa Mungu anayejua wapi umetoka na wapi unaenda?

Yeremia 1:5
Mungu akisha kutambua inatosha sana haijalishi umetokea wapi bali vile Mungu alivyo kwako.

Zaburi 51:5


Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com




“Itakuwa vizuru tukikutana tena katika wakati mwingine………..BARIKIWA