VIGEZO VYA KUMPENDA
MUNGU (UTHIBITISHO)
Hili ni jambo la kawaida sana kwa mtu yeyote mtu
utakaye mpenda lazima awe na sifa ambazo wewe unazozitaka na wala haiwezi
kutokea wewe hali ya kupenda penda hovyohovyo mtu asipite mbele zako.
Mungu apendwi kwa kuwa umejisikia kumpenda au umeona
tu ipo haja ya kumpenda kwa wakati Fulani,bali viko vitu ambavyo Mungu akiviona
anajua tu wewe sasa umeamua kumpenda kwa dhati sio unajaribu kumpenda.Katika
kitu kizuri Mungu hashawishiki kwa maneno ya kawaida tu bali moyo unao jua
unachofanya ndio unao mtisha Mungu.
Sio kwa vigezo vyako ndio ukaweze kumshawishi Mungu
akupende bali ni kwa vigezo vyake, ikiwa kwa ni kwa vigezo vyako basi
utajipenda mwenyewe na kama kwa vigezo vyake basi yeye atakupenda.
i.maisha
ya kuacha vyote kwa ajili ya kristo kwa ukamilifu
unapoamua kumfuata yesu uyashikilie hayo maamuzi
ulio yachukua na moyo wako ukushuhudie pasipo shaka ndani yako.
Ni jambo la muhimu kwa watu wanao amua kupendana ili
waweze kuzidi na kushamili lazima asiwepo mtu mwingine akawa na nafasi sawa
ndani yenu kama mlivyo.
Hali ya kuacha vyote haimaanishi kwamba uache kusoma
kama unasoma,kuacha kazi kama unafanya kazi
au una fanya shughuli yeyote ya halali ukaiacha sivyo.
Bali ni vile moyo wako unavyo yapa kipaumbele/uzito
mambo ambayo yanamfanya Mungu kuzidi ndani ya maisha yako.
Tamani sana maisha yako yawe na muunganiko wa kweli
na Mungu yenye utiisho,mamlaka na nguvu pamoja na ushindi.
Tamani kuona maisha yako yakimuonyesha Mungu katika
mwenendo mzima ulionao watu waone huruma,upendo,uponyaji,uweza wa Mungu penda
kuona Mungu akiyafurahia maisha yako kuliko mtu yeyote hata mpenzi wako.
Mathayo 16:24-25
Kubali yote ya kukute lakini kamwe yasivuruge Mungu
katika maisha yako yakaleta utengano wako na Mungu.
Yohana 16:27
ii.maisha
ya kuangalia Mungu anakuonaje na wala sio wanakuonaje?
Siku zote motto mwenye akili uangalia wazazi wake
wapendacho na si majirani wanachosema kwakua utambua furaha ya wazazi ndio
furaha yake.
Mithali 10:1
siku zote watu wanakuona vile unavyoonekana hawa
wezi kukuongeza au kukupunguza bali nafasi yao ni kusema katika hali ya kukosoa
au kupongeza kulingana na mtazamo wake.
Una haja ya kuogopa hao bali unao nafasi ya
kuwasikiliza na kuwa heshimu lakini mmbo mengine yote yana baki ndani yako
binafsi kwani wewe ndio unajipenda hasa kuliko mwingine.
Maisha yasiyo ambatana na hofu ya kibinadamu bali ni
hofu ya Mungu iliyo katika hali ya kupenda tena kwa furaha.
Maana Mungu katika wengi anakuangalia wewe binafsi
hivyo katika wengi muangalie yeye binafsi.
Mhubiri 7:26(b)
Luka 12:22-24
iii.maisha
yasiyo tazama aibu ya sasa bali aibu ya baadae(aibu ya milele)
Ishi maisha ya kutopata aibu ya milele kuliko aibu
ya sasa isiyo dumu, hatima ya wanadamu iko mikononi mwa MUNGU.
Mathayo 10:32-33
Luka 12:20-21
Hakuna kisichikuwa na mwisho katika ulimwengu huu
bali ni NENO LITOKANALO KINYWANI MWA MUNGU.
Ishi isha ambayo kishindo cha mbingu kitaitikia na
kukukubali na kusema kweli wewe ni mtu uliye amua kumpenda Mungu.
iv.maisha
ya kufungwa nira ya kristo
haya ni maisha ya kumjua zaidi kristo kuliko
chochote kwa kuwa ndicho kilichopewa nafasi kubwa ndani ya moyo mwake.
Unaposikia kitu kinachoitwa Mungu moyo wako
unashtuka haoni nafasi ya kutulia kwa kuwa hauoni jambo ambalo litazuia kitu
chochote kitazuia upendo wako kwake.
Moyo wako hutamani/haupendi kuona akisijisikia
vibaya kwa ajili yako wewe unatamani kuona siku zote anakuwa na furaha pindi
anapoona uwepo wako.(wewe ndio furaha yake)
Matendo 15:26
Mathayo 11:28-30
Utayari wako uwe kwaajili ya Mungu tu kwa ukamilifu
wote mtumikie bwana wako pasipo shaka yoyote tena katika hali ya furaha
isiyokoma.
Matendo 21:13
v.maisha
ya kujenga mwili wa kristo
Na wala sio maisha yanayowaza kwa ajili yake binafsi
bali ni mawazo yaliyojaa nimfanyie nini Mungu leo kizuri kuliko jana, hii ni
hali muhimu sana kwa watu wanaopendana uwa wanawaza kwa ubora siku kwa siku
unaongezeka.
Unatamani kuona furaha yake ikizidi siku hadi siku
na sio ipungue ili linakuwa ni jukumu lako kwa kuwa UNAMPENDA.
Huu ndio moyo ambao Mungu anautafuta ambao
utasimamisha ufalme wake na kuimalika na kuwa wakumu usio tikisika milele.
Mathayo 16:18
Waefeso 4:11-12
Unajenga mwili wa kristo kwa njia ya PENDO LA MUNGU NDANI YAKO.
Imeandaliwa na ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
KILA LA KHERI…………..RAFIKI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni