Jumatatu, 16 Septemba 2013

KIJANA WA MAANA YU KOJE?



KIJANA WA MAANA:

Katika kuendelea juu ya kuwa kijana wa maana mbali na kuwa na pesa tu na vitu vingi vinaonekana vya thamani kwa mwanadamu.tunapenda tena tuangalie katika kipengele kinachofuata.
                                          

                                              II.Maisha uliyopitia (mateso & shida)

Maisha ni mchangunuo wa mambo mbalimbali ambayo mwanadamu anapitia tena katika hali tofautitofauti ambayo mwanadamu anapitia kila maisha mtu binafsi aliyopitia uacha alama ndani ya moyo wako na kuwa ni elimu kwa mtu husika au uzoefu alioupata katika maisha yake.

Katika sayari ya dunia tuliyonayo sasa wapo watu amabao wanaishi maisha tofautitofauti katika hali nzuri/njema na hali mbaya/duni.pia wako watu walianzia hali njema baadae wakaishia pabaya na wengine wapo walioanzia katika hali mbaya baadae wakaishia katika hali nzuri/njema na wengine wamekuwa na mchanganyiko na hatimae wakaishia katika hali iliyo njema au iliyo mbaya, inategemea na familia uliyotoka pamoja na hayo pia kuna kundi la watu ambao maisha yao ni maumivu mwanzo mwisho.

Na maisha uliyoyapitia ndio leo uko vile ulivyo katika muonekano ulionao sasa wa huzuni au wa furaha.
Hakuna maisha ambayo uliyo yapitia mbali na wokovu yakawa na kibali kwa Mungu kwa namna yoyote haijalishi jamii inakukubali au haikukubali katika muonekano wowote wa dunia hii hauna kibali kwa Mungu bali ni vile Mungu anavyotaka tu ndivyo utaupendeza moyo wa Mungu.

Unapoishi maisha mbali na wokovu unakuwa unajifunza vitu vingi na kushiriki mambo ambayo yanawezekana kuonekana katika ubora wake katika jamii yako jua jambo lolote unalojifunza au kushiriki lina jenga mambo ambayo yataendesha maisha yako katika namna unavyoelewa.

Na pindi usipokuwa makini unaweza kujikuta katika hali tete ambayo itakusumbua katika maisha yako inaweza kuwa kikwazo kati yako na Mungu kwa kiasi kikubwa na yanaweza kuwa kikwazo kikubwa katika kuleta maendeleo yako katika maisha ya rohoni na ya mwilini.


Kama binadamu wakawaida kuna yako mambo uliyokuwa unayafanya unapokuwa pekee yako chumbani au mahali popote pa siri(kufanya mapenzi, kujichua, mawazo ya ukatiri na dhana ya kutaka kujiua)


I wathesalonike 4:3-5

Kuna muonekano ambao Mungu alikusudia katika kutimiza hazma yake katika kukuleta hapa dunia kuna namna ya wewe kuwa usiwe tu kiolela. Kama baba aliye makini anavyoweza kumwandalia mwanawe hatma njema ya baadae.

Luka 12:2-3

Muonekana wako wa awali unaonekana sasa kwa kuwa vile utakavyo ishi itategemea sana vile unavyoelewa na kukubaliana na hali uliyokuwa nayo hapo awali.

II Samweli 12:12

I Wakoritho 6:13-20

Mwanzo 8:21

Mambo yoyote yanapokuwa yakiendelea katika nafsi ya mtu husika na wakati wingine mtu huyu uweza kutekeleza yale yanayoendelea ndani yake.

Na pindi unapojaribu kutenda jambo hili kuna mambo yanazaliwa kutokana na tendo hilo ambayo yanakuwa na muonekano mbalimbali:

Hesabu 31:17-18
                   
                    i)kuna hali ya kushutuka pindi mambo hayo yanapotamkwa.
  
 ii) hofu na kutojiamini utawala na kuwa na nafasi katika maisha ya muhusika.
           
 iii) hali ya wasiwasi na mashaka juu ya magonjwa ya zinaa mathalani. Ukimwi ,kisonono na mengine mengi.
          
 iv) wengine wana kuwa na hali ya ukimya na wengine inawatokea hali ya kupenda kuongea pasipo sababu.
         
 v) kuchukia haina ya jinsia inaweza kuwa ya kike au ya kiume.
          
vi) mawazo sugu ambayo yamekosa muafaka.
         
vii) kutoa mimba( lina hasara kubwa katika maisha ya mtu husika)

Ni vizuri kutafakari wapi umetoka na je! Unaenda wapi na je! Utafika je, hiyo safari yako uwezekano wa kufika upo kwa kiasi gani na uko tayari katika chngamoto mbalimbali katika kufikisha ile hatma yako.

Ni vizuri kutambua kuwa unahitaji neema ya Mungu katika kukufikisha pale ambapo yeye mwenyewe amepanga na kukusudia ya kuwa wewe upate kufika mahali husika na sio pale ambapo unatamani wewe tu.

Hii iko wazi ujana ili uweze kuwa mzuri au mbaya unategemea sana nani ni kiongozi wako katika kuongoza maisha yako.

Yohana 10:10
Mbali na Mungu hakuna ujana ulio salama kama ujampa yesu maisha yako kwa ukamilifu wake hauwezi ukawa salama.

Isaya 40:28-31
Hakuna mtu anajua jinsi unavyotakiwa kuwa isipokuwa Mungu anayejua wapi umetoka na wapi unaenda?

Yeremia 1:5
Mungu akisha kutambua inatosha sana haijalishi umetokea wapi bali vile Mungu alivyo kwako.

Zaburi 51:5


Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com




“Itakuwa vizuru tukikutana tena katika wakati mwingine………..BARIKIWA

Jumatatu, 9 Septemba 2013

KIJANA WA MAANA YUKOJE?



KIJANA WA MAANA;

Sehemu ya pili……………

Karibu katika sehemu yetu yakuzungumza kuhusu kijana namna gani ili kuwa wa maana mbele za Mungu na mbele za jamii yako inayokuzunguka. Tutajadili kwa pamoja na ikiwa una maoni usisite kutuandikia kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

Leo kama siku ambayo Mungu ametupa neema yake ya mimi na wewe kukutana tena kwa njia hii ya maandishi tutakwenda kuangalia katika sehemu inayofuata:
                                                        

                                                            I(b)Makuzi gani umepitia?

Zaburi 11:3

Kila mtu ana mahali alipotoka na mahali hapo pame mweka kuwa vile alivyo leo hivyo ni muhimu sana kutambua katika makuzi uliolelewa na ndiyo yaka kutengeneza wewe ulivyo leo na lasivyo usingekuwa wa leo tunae kufahamu.

Yako mambo ambayo umepitia katika makuzi yako,mathalani kukeketwa(unyago),kubakwa kutengwa(kunyimwa haki) au maisha ya majonzi kama vile kufiwa yote haya katika kukufanya kuwa kijana wa maana au mtu unayethaminika hapo baadae. Kwa hakika jana yako ndio msingi wa leo yako.

Jamii kwa ujumla wake ambao hawamjui Mungu wa kweli hawakukupokea vile utakiwavyo kwa ufasaha zaidi isipokuwa walikupokea kwa namna yao na hata makuzi yao katika misingi ambayo waliona ni mizuri kwao na pengine wasioone hiyo misingi kwa Mungu ina nafasi gani?

Ni jamii chache sana ambao waliopokea watoto wao katika misingi ya ki Mungu lakini kwa asilimia kubwa tulilelewa katika misingi isiofaa(ulevi,migogoro katika ndoa na hata kuteswa) na baadhi yetu tumejilea wenyewe kwa hiyo misingi tuliyo nayo imejengwa na sisi wenyewe au kwa ushawishi wa watu ambao tulio kuwa pamoja nao.

Kuna namna ya walivyo kuandaa kupambana na maisha yaliyo mbele yako mfano.unyago na jando(kwa waliopitia) au maneno ambayo wamekwambia namna ya kuenenda kama mwanamke au mwanaume ambayo ya kukuonyesha wewe ni nani katika jamii inayokuzunguka.

Inawezekana ulipitia katika uchawi au ushirikina hata kufundishwa ukatiri kwa yale uliopitia haya mambo yote yana weka giza au kutofika katika maisha yako.

Vile ulivyo inategemea sana misingi uliyo kuwa nayo na  kule utakavyo enda bado inategemea sana misingi uliyokuwa nayo.

Vile ulivyo ndivyo utakavyo warithisha wale walio mbele yako utawaacha katika misingi ipi ambayo itawasaidia au kuwaangamiza.

Prepared by ;
                    Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com

                 

                           “Tukutane wakati mwingine…………..barikiwa!!!!”

Jumatatu, 2 Septemba 2013

KIJANA WA MAANA YUKOJE?



KIJANA WA MAANA:

Sehemu ya kwanza……………………………

Kijana kuwa wa maana hiyo ndio kiu ya watu waliokatika rika hili na ndo maana wanatumia wakati wao mwingi kujishughulisha ili mwisho wa siku wawe wa maana katika nyanja zote za kimaisha, na pindi anaposhindwa kutimiza hazma hii uwa moyo wake unakuwa mnyonge sana na hatimae uweza kufikia maamuzi ambayo yanaweza hatarisha maisha yake kwa kiasi kikubwa sana baadhi yao uweza kujiingiza katika madawa ya kulevya, vitendo vya ngono na matendo ambayo yanayo hatarisha maisha yao na hata kuvunja sheria za nchi.


Kwa uhakika kijana ni hatua  ambayo inaaminika ni hatua ya mabadiliko, kwahiyo ni hatua ambayo unahitaji uangalifu mkubwa katika kufanya maamuzi sahihi.

Kuna mifano mingi ya watu ambao walio fanikiwa lakini wamejenga misingi mizuri tangu ujana wao na hatimae kuja kuvuna yale ambayo hatua inayofuata.

Kutokana na maelezo ya hapo awali tutakwenda kujifunza hatua kwa hatua kuhusu kijana na hatimae tumpate kijana wa maana.

Napenda kuzungumzia mapema sana tunapozungumzia kijana wa maana hatuzungumzii muonekano mzuri(physical appearance) au kuvaa mavazi ya gharama sana.
UJANA ni hatua ya tatu(biology) ambayo kila mwanadamu anapitia ili kufikia hatua ya uzee(utu uzima). Ni hatua mbayo watu ambao wanapata neema kufikia huwa wanapenda kudumu katika hatua hii pasipo kutaka kwenda hatua ya uzee.
Mithali 20:29@

Kama kipindi ambacho unaweza kuifaidi dunia kwa namna ya kipekee ni hatua hii kwani unakuwa unaweza kufanya mengi na ukakizi haja yako na kutokana na uwezo wako katika uchumi au uimara wa mwili wako.
Hii nafasi ambao haijurudii jambo ambalo ulitakiwa kulifanya kipindi usitegemee kulifanya katika hatua nyingine kwakua kila hatua kuna mambo yake.


Tutakwenda kuangalia mambo mbalimbali ambayo yanaweza fanya ujana kuharibika;
                               I.wapi umezaliwa? Makuzi(kulelewa) gani umepitia?
                               II.maisha gani umepitia?
                               III.uhuru uliopewa na maamuzi uliyofanya.

                                                           
                             I.(a)wapi umezaliwa?

Kila mwanadamu anachimbuko lake japo anaweza kulijua au kutolijua kutokana sababu mbalimbali ila kubwa sana lakutambua vile chimbuko lilivyo ndivyo ulivyo, kwakua wewe  ulivyo unawakilisha chimbuko lako na kamwe hauwezi kuwakilisha chimbuko ambalo si lako hivyo njia nzuri ya kutoka mahali ni vizuri wapi umezaliwa kwakua mahali ulipo zaliwa panajenga msingi katika maisha yako unategemea ukawa mzuri au ukawa mbaya, ni wazi ubora mti utegemea shina lilivyo na sio matawi wala jambo jingine.

Kila jamii husika ina namna ya kumchukulia mtoto au kijana kutokana na misingi ya jamii husika na sio kama jamii nyingine.

Namna wanavyo mpokea mtoto unajengwa na mtazamo wao wakufanya jambo hilo ambao unaweza kuwa umejengwa na misingi ya kikabila katika mila na desturi.
Hakuna kabila ususa afrika yetu inayo mpokea mtoto  katika misingi ya kumjua Mungu na kumfanya ampende Mungu maisha yake yote, bali watu ufikiria namna ya kumfanya hayafurahie maisha yake hapa duniani pasipo kuhofia maisha yaliyopo baada ya kutoweka duniani.
Mwanzo 6:5
II wafalme 21:1-12
II wafalme 22:24-26
Maisha ya wazazi yametawaliwa na hofu kuhusu hatma ya watoto wao kwani matazamio ya wazazi hawa ni kuona ustawi wao wangalipo duniani na hata wa kizeeka wapatwe kutunzwa hivyo uwabidisha katika kuwafanya wawe na mwelekeo ulio bora wa maisha yao hapa duniani hili silo tatizo kwa kua mafanikio ya mtoto ndio furaha ya mzazi na kushindwa kwa mtoto ndio aibu kwa wazazi.
Pamoja na hayo yote ni vizuri kutambua kwa mtoto wako ili aweze kuishi vyema hapa duniani ni muhimu sana aweze kuishi huku akimjua Mungu muumba dunia na elimu katika kupanua ufahamu haifahamu dunia katika namna ya kibinadamu.

Pale ulipo zaliwa panaweka nuru au giza katika maisha yako ya baadae kwa hiyo shina lina hamua uishi vipi hapa duniani katika hali njema au ya mateso.
Ayubu 14:4
Kutoka 20:5
Waebrania 7:9-10

Yale maneno unayoambiwa tangu mtoto yanajenga vitu katika maisha ambayo athari zake utaanza kuziona mara baada tu ya kuanza kutawala maisha yako. Mathalani watoto wa kipalestina wanaopandikizwa chuki dhidi ya waisraeli hayo maneno yanakuwa na nguvu na kusimama kutoa mwelekeo wa maisha yako.
Usipopata msaada utaangamia na usipo kuabali kupokea huo msaada bado utaangamia.

Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com



                                Asante tukutane wakati wakati ujao…………………..!!!!!!!!!