KIJANA WA MAANA:
Katika kuendelea juu ya kuwa kijana wa maana mbali
na kuwa na pesa tu na vitu vingi vinaonekana vya thamani kwa
mwanadamu.tunapenda tena tuangalie katika kipengele kinachofuata.
II.Maisha uliyopitia (mateso & shida)
Maisha ni mchangunuo wa mambo mbalimbali ambayo
mwanadamu anapitia tena katika hali tofautitofauti ambayo mwanadamu anapitia
kila maisha mtu binafsi aliyopitia uacha alama ndani ya moyo wako na kuwa ni
elimu kwa mtu husika au uzoefu alioupata katika maisha yake.
Katika sayari ya dunia tuliyonayo sasa wapo watu
amabao wanaishi maisha tofautitofauti katika hali nzuri/njema na hali
mbaya/duni.pia wako watu walianzia hali njema baadae wakaishia pabaya na
wengine wapo walioanzia katika hali mbaya baadae wakaishia katika hali
nzuri/njema na wengine wamekuwa na mchanganyiko na hatimae wakaishia katika
hali iliyo njema au iliyo mbaya, inategemea na familia uliyotoka pamoja na hayo
pia kuna kundi la watu ambao maisha yao ni maumivu mwanzo mwisho.
Na maisha uliyoyapitia ndio leo uko vile ulivyo
katika muonekano ulionao sasa wa huzuni au wa furaha.
Hakuna maisha ambayo uliyo yapitia mbali na wokovu
yakawa na kibali kwa Mungu kwa namna yoyote haijalishi jamii inakukubali au
haikukubali katika muonekano wowote wa dunia hii hauna kibali kwa Mungu bali ni
vile Mungu anavyotaka tu ndivyo utaupendeza moyo wa Mungu.
Unapoishi maisha mbali na wokovu unakuwa unajifunza
vitu vingi na kushiriki mambo ambayo yanawezekana kuonekana katika ubora wake
katika jamii yako jua jambo lolote unalojifunza au kushiriki lina jenga mambo
ambayo yataendesha maisha yako katika namna unavyoelewa.
Na pindi usipokuwa makini unaweza kujikuta katika
hali tete ambayo itakusumbua katika maisha yako inaweza kuwa kikwazo kati yako
na Mungu kwa kiasi kikubwa na yanaweza kuwa kikwazo kikubwa katika kuleta
maendeleo yako katika maisha ya rohoni na ya mwilini.
Kama binadamu wakawaida
kuna yako mambo uliyokuwa unayafanya unapokuwa pekee yako chumbani au mahali
popote pa siri(kufanya mapenzi, kujichua, mawazo ya ukatiri na dhana ya kutaka
kujiua)
I wathesalonike 4:3-5
Kuna muonekano ambao Mungu alikusudia katika
kutimiza hazma yake katika kukuleta hapa dunia kuna namna ya wewe kuwa usiwe tu
kiolela. Kama baba aliye makini anavyoweza kumwandalia mwanawe hatma njema ya
baadae.
Luka 12:2-3
Muonekana wako wa awali unaonekana sasa kwa kuwa
vile utakavyo ishi itategemea sana vile unavyoelewa na kukubaliana na hali
uliyokuwa nayo hapo awali.
II Samweli 12:12
I Wakoritho 6:13-20
Mwanzo 8:21
Mambo yoyote yanapokuwa yakiendelea katika nafsi ya
mtu husika na wakati wingine mtu huyu uweza kutekeleza yale yanayoendelea ndani
yake.
Na pindi unapojaribu
kutenda jambo hili kuna mambo yanazaliwa kutokana na tendo hilo ambayo yanakuwa
na muonekano mbalimbali:
Hesabu 31:17-18
i)kuna hali ya kushutuka
pindi mambo hayo yanapotamkwa.
ii) hofu na
kutojiamini utawala na kuwa na nafasi katika maisha ya muhusika.
iii)
hali ya wasiwasi na mashaka juu ya magonjwa ya zinaa mathalani. Ukimwi
,kisonono na mengine mengi.
iv)
wengine wana kuwa na hali ya ukimya na wengine inawatokea hali ya kupenda
kuongea pasipo sababu.
v) kuchukia haina ya jinsia inaweza kuwa ya
kike au ya kiume.
vi) mawazo sugu ambayo yamekosa muafaka.
vii) kutoa mimba( lina hasara kubwa
katika maisha ya mtu husika)
Ni
vizuri kutafakari wapi umetoka na je! Unaenda wapi na je! Utafika je, hiyo
safari yako uwezekano wa kufika upo kwa kiasi gani na uko tayari katika
chngamoto mbalimbali katika kufikisha ile hatma yako.
Ni
vizuri kutambua kuwa unahitaji neema ya Mungu katika kukufikisha pale ambapo
yeye mwenyewe amepanga na kukusudia ya kuwa wewe upate kufika mahali husika na
sio pale ambapo unatamani wewe tu.
Hii
iko wazi ujana ili uweze kuwa mzuri au mbaya unategemea sana nani ni kiongozi
wako katika kuongoza maisha yako.
Yohana 10:10
Mbali
na Mungu hakuna ujana ulio salama kama ujampa yesu maisha yako kwa ukamilifu
wake hauwezi ukawa salama.
Isaya 40:28-31
Hakuna
mtu anajua jinsi unavyotakiwa kuwa isipokuwa Mungu anayejua wapi umetoka na
wapi unaenda?
Yeremia 1:5
Mungu
akisha kutambua inatosha sana haijalishi umetokea wapi bali vile Mungu alivyo
kwako.
Zaburi 51:5
Prepared by ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
“Itakuwa vizuru tukikutana tena
katika wakati mwingine………..BARIKIWA”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni