Jumatano, 31 Julai 2013

MAARIFA YENYE MAFUTA YA KIMUNGU



MAARIFA YENYE MAFUTA YA KIMUNGU:

Ukisikia mtu anatafutwa ujue anakitu kinachofanya atafutwe, wakati mwingine anaweza asionekane sana lakini pindi anapohitajika basi hapo anakuwa lulu.
Mfano.mfalme Suleiman alikuwa anatafutwa na watu wengi wenye hadhi kubwa na ndogo kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Mtu anaweza kuwekwa au kuonana na watu wakubwa ulimwenguni (maraisi, mawaziri na watu wenye uwezo tofautitofauti)
Ni bora ukose Mali na vitu vya thamani vinavyoonekana kuliko upate vyote halafu hukose maarifa yenye mafuta ya kimungu.
Mfano.suleimani aliomba hekima toka juu na vingine vikaja pasipo kuomba wala kufunga bali bwana alionauhitaji akatoa.
Lazima akili yako isielewe bali Roho mtakatifu ahieleweshe.
Kunatofauti kubwa sana kati kuwa na maarifa na kuwa na maarifa yenye mafuta ya kimungu. Havifanani wala havifananishwi.
Hivyo ujue hauhitaji maarifa bali unahitaji maarifa yenye maongozi ya Roho mtakatifu.
Maarifa haya yanazaliwa na Roho mtakatifu toka ndani yako ila kama unae na umempa nafasi ya kutosha.
Utofauti mkubwa kati yako na wadunia ni kutembea katika maarifa yenye mafuta ya kimungu tofauti ya hapo hakuna utofauti. Ulio wa maana mbele za Mungu.

FAIDA YA KUWA NA MAARIFA YENYE MAFUTA:

I. nguvu ya kusimamia hadhina ya kimungu.
Namna unavyosimamia hadhina ya Mungu ndivyo unavyo jenga msingi wa mafanikio yako.

II .nguvu ya kusikia sauti kuliko mambo mengine.
Ushabiki na mbwembwe kukosa nafasi ndani yako unavyosikia na kuchukua hatua ni Mungu anachukua maamuzi.


Prepared by ;
                  Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com 
                      
                   Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com