KIJANA WA MAANA;
Sehemu ya pili……………
Karibu katika sehemu yetu yakuzungumza kuhusu kijana
namna gani ili kuwa wa maana mbele za Mungu na mbele za jamii yako
inayokuzunguka. Tutajadili kwa pamoja na ikiwa una maoni usisite kutuandikia
kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
Leo kama siku ambayo Mungu ametupa neema yake ya
mimi na wewe kukutana tena kwa njia hii ya maandishi tutakwenda kuangalia
katika sehemu inayofuata:
I(b)Makuzi gani umepitia?
Zaburi 11:3
Kila mtu ana mahali alipotoka na mahali hapo pame
mweka kuwa vile alivyo leo hivyo ni muhimu sana kutambua katika makuzi
uliolelewa na ndiyo yaka kutengeneza wewe ulivyo leo na lasivyo usingekuwa wa
leo tunae kufahamu.
Yako mambo ambayo umepitia katika makuzi yako,mathalani
kukeketwa(unyago),kubakwa kutengwa(kunyimwa haki) au maisha ya majonzi kama
vile kufiwa yote haya katika kukufanya kuwa kijana wa maana au mtu
unayethaminika hapo baadae. Kwa hakika jana yako ndio msingi wa leo yako.
Jamii kwa ujumla wake ambao hawamjui Mungu wa kweli
hawakukupokea vile utakiwavyo kwa ufasaha zaidi isipokuwa walikupokea kwa namna
yao na hata makuzi yao katika misingi ambayo waliona ni mizuri kwao na pengine
wasioone hiyo misingi kwa Mungu ina nafasi gani?
Ni jamii chache sana ambao waliopokea watoto wao
katika misingi ya ki Mungu lakini kwa asilimia kubwa tulilelewa katika misingi
isiofaa(ulevi,migogoro katika ndoa na hata kuteswa) na baadhi yetu tumejilea
wenyewe kwa hiyo misingi tuliyo nayo imejengwa na sisi wenyewe au kwa ushawishi
wa watu ambao tulio kuwa pamoja nao.
Kuna namna ya walivyo kuandaa kupambana na maisha
yaliyo mbele yako mfano.unyago na jando(kwa waliopitia) au maneno ambayo
wamekwambia namna ya kuenenda kama mwanamke au mwanaume ambayo ya kukuonyesha
wewe ni nani katika jamii inayokuzunguka.
Inawezekana ulipitia katika uchawi au ushirikina
hata kufundishwa ukatiri kwa yale uliopitia haya mambo yote yana weka giza au
kutofika katika maisha yako.
Vile ulivyo inategemea sana misingi uliyo kuwa nayo
na kule utakavyo enda bado inategemea
sana misingi uliyokuwa nayo.
Vile ulivyo ndivyo utakavyo warithisha wale walio
mbele yako utawaacha katika misingi ipi ambayo itawasaidia au kuwaangamiza.
Prepared by ;
Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
“Tukutane
wakati mwingine…………..barikiwa!!!!”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni