Jumanne, 27 Agosti 2013

je! mavazi yana nafasi gani katika ukristo



                                                             MAVAZI;

Mavazi ni gumzo katika jamii yetu tuliyonayo imeathiri heshima ya mtu kwa aliye muhusika,Yule aliye vaa vizuri basi uheshimiwa kutokana na muonekano na alivaa isivyo onekana vyema basi heshima kwa mtu huyo upotea.
Wako watu wanakosa uhuru kutokana na hali hii, je! Vazi sahihi kwa mtu ni lipi na kwanini likawa lile na lisiwe hili.
Jambao hili limekuwa ni tatizo ikitegemea na familia husika au jamii husika kwa wakati familia moja inatoa ruhusa juu ya vazi Fulani na jamii nyingine inakataza. Hivyo hali hii inategemea jamii husika kwakua ndani ya jamii kuna mgawanyiko wapo wana wanakubali na jamii nyingine hawakubali.
Wako watu ambao wametengwa na jamii katika huduma kama vile kanisani,hospitali na maeneo mengine kwa sababu ya mavazi.


Katika kujadili jambo hili yako mambo inabidi tuyaangalie:
                               (a)Je! Nguo inawezekana kuwa tatizo katika ukristo.
                               (b)Je! Nguo inamchango wowote katika kufanya ibada.
                             (c)unafikiri Nguo inaweza kutoa picha ya mkristo(ushuhuda) kwa waliookoka na wasio okoka.
          Katika kuangalia kwa utangulizi tatizo linaweza kuwa pande zote mbili kutokana na mitazamo tofauti iliyoko ndani ya jamii yetu,
-kwa nini mtu binafsi ameamua kuvaa(msukumo gani umepelekea kuvaa vile ulivyo vaa) na anayekutazama kwa nini amefikia hapo(mtazamo gani aliokuwa nao ikampa tafsiri hiyo ambayo mtu binafsi ameiamini)
2 samweli 13:18
Ni kweli Mungu ashughuliki na muonekano wanje bali NIA YAKO katika muonekano wako. Hiyo  inawezekana hali hiyo kuwa shida kwa jamii lakini si kwa Mungu, kwakua muonekano wako haumbadilishi Mungu mtazmo wake kwako  bali inaweza kuwa najisi kwa watu.
Ni kweli unaweza kuvaa vizuri katika muonekano wowote lakini bado usiwe ushuhuda mzuri kwa jamii japo katika hali hii bado hatuamasishi kuvaa kwa muonekano usio sawa.
Kwa mkristo ambaye anaye thamini ukristo wake sio mbaya kwenda na wakati(kuwa wa kisasa) lakini huo upya usiishie kwenye mavazi na mapambo katika mwili wako tu bali jitaidi hata katika utu wako wa ndani(mahali ambapo unaanda hatma yako katika Mungu) kwakua Roho mtakatifu anaweza akakupa hekima namna ya muonekano sahihi na kauli ya kuwajibu watu.
Ipetro 3:2-5,6-
Pamoja na hayo yote jua kuna nafasi ya wewe binafsi ya kujistiri kwakua wewe si kama mnyama hivyo unahitaji kuwa katika nafasi ambayo utaongeza marafiki na wala si maadui.
                                      

                           (a)Je! Nguo inawezekana kuwa tatizo katika ukristo.
Kwa upande wa Mungu hakuna shida kwakua mavazi yako haya mfichi Mungu asione utupu wako ila namna ya unavyo vaa inaweza kuwa tatizo kwa binadamu wanao kuzunguka.
Ni vizuri kutambua kuwa unapishana na watu na pia unakaa  na watu zaidi sana unawahitaji watu hivyo usipo wafanya wakufurahie jua kuna wakati utakapo wahitaji inawezekana historia ikasema ndani ya maisha yako.
Pindi unapokuwa sehemu Fulani kunautaratibu wake iwe ofisini,shambani n.k mathalani shuleni kuna namna utavaa kwa namna taratibu za shule zinavyo ruhusu na utavaa si kwamba unapenda kuvaa hivyo wakati mwingine inakulazim kuvaa hivyo kwakua unahitaji elimu na mambo mengi yaliyo mema.
Sikuzote tambua unaishi katika dunia ambayo uliwakuta watu wakiishi hivyo unapoenda nje ya utaratibu usitegemee jamii ikakukubali.
“mwanamke apaswi kuvaa mavazi yampasayo mwanaume”
Torati 22:5

Katika yote tunatambua kutokana na biblia inavyosema hakuna uhusiano ulio kati ya Nguo na Mungu isipokuwa Moyo wa mtu na Mungu ili ni muhimu kutangulia kulitambua.
Pamoja na hayo yote ni vizuri kuishi na watu vizuri na katika hali stahiki na pindi utakapo ona nguo ni kikwazo katika jamii badilika sio kwa sababu unawaogopa bali kwa sababu unawapenda wao na Mungu.
Waebrania 12:14
Tambua uwepo wa watu hao ndio unakupa umaana wewe kuwepo dunia peke yako itakuboa na haita leta maana na kufanya kuboreka. Hivyo jua unahitaji watu basi hakikisha uwepo wako ulete furaha kwao.
Usione ngumu kubadilika kwakua mazoezi mazuri yatakufanya uwe vizuri ukiamua unaweza, kwakua Mungu yupo kwa ajili ya kukuwezesha kuwa mtu wa maana mbele yake na hatimae mbele za wanadamu.(kwakua hakuna jambo la kumshinda Mungu).
Akili yako inahusika sana kwakua ndani ya akili ni ufunguo wa utendaji wako  hapa duniani akili ikibadilika basi ujue na wewe umebadilika.
Ni vizuri kutambua kuwa unao uwezo wakubadilika na jamii ikakukubali.
Paulo anasema…….
“nilivyoenda kwao nilikuwa kama wao”
Kwakua unatambua mavazi hayana ushirika na Mungu bali ni moyo wako na Mungu basi inawezekana kuacha mavazi ambayo ni kikwazo kwa watu wengi ila ukaendelea ukang’ang’ania ushirika wako na Mungu ndicho cha msingi kwako.
Ni vizuri kuhakikisha watu na Mungu wanafurahishwa katika uwepo wako.
“yesu akakua akimpendeza Mungu na wanadamu…….”
Luka 2:52
Ni kweli hata ukibadilika ukawa sawa na jamii unavyokutaka wako watu bado hauta pata kibali kwao ilo usijali ugomvi wachie Mungu na wao.

                              
                                (b)Je! Nguo inamchango wowote katika kufanya ibada.
Ibada na nguo ni vitu viwili tofauti, nguo ni kwa ajili ya mwili tu na ibada ni jumla ya mambo yote yanaendelea ndani ya moyo wa mwanadam.
Japo mavazi yana maana mbalimbali kuna mavazi ambayo watu huona vema wayavae ofisini na kuna mavazi ambayo watu wanaona wa yavae sehemu za ibada na maeneo mengine kadili jamii husika ilivyoona vyema.
Hata katika biblia mavazi yalikuwa yana valiwa kutokana kazi husika, jinsia na hata rika gani linatakiwa livaeje?
-Watu walikuwa wanafua nguo ilikukutana na Mungu hivyo unadhifu na umaridadi ulikuwa unazingatiwa
Makuhani walikuwa na nguo(naivera) ambayo waliitumia katika kupeleka ibada kwa niaba ya wanaisrael.
Ni kweli nguo ni nguo na Mungu ni Mungu lakini pamoja na hayo unahitaji mambo ambayo yatakuwa msaada kwako katika kuimairisha mausiano kati yako na Mungu na binadamu;

Vaa nguo ambayo utaifurahia.
Vaa nguo ambayo itakuweka uwe huru ambayo haita toa staili ya kuenenda au kukaa jambo hili unaweza kuona ni jambo la kawaida lakini linaweza kukuweka kutofanya uhuru mbele za Mungu vilevile anahitaji mwili wake hutumie kwa ajili yako kwa maana hilo ni hekalu la Mungu.
I wakorintho 6:19
Ili ni ngumu kwa akili ya kibinadam unahitaji moyo utengenezwe na neno la Mungu ili uwe tayari kuyafanya hayo.( ni vizuri kujua kuwa unahitaji umfurahishe Mungu ili yeye akutane na mambo yako).
-ni muhimu kuvaa nguo ambayo haita kamata akili yako kiasi kwamba utashindwa kumwabudu Mungu na kumsifu yeye.
-vilevile hakikisha hiyo nguo isikupe mashariti jinsi ya kucheza kwa bwana.
Ukweli nguo si shida lakini inaweza kuchangia katika kuchafua moyo wako mwisho ikakupelekea kutoifurahia ibada napengine hata ukajuta kwanini umeivaa hiyo nguo.


                             (c)unafikiri Nguo inaweza kutoa picha ya mkristo(ushuhuda) kwa        waliookoka na wasio okoka.
Hata kama haitatoa au kutoa lakini ni vizuri uonye kuitambua jamii yako na kuipenda katika udhati.
Japo ni kweli kwamba hakuna kwa aina yoyote ya nguo ambayo yesu huitumia kufanya mambo yake bali mtu husika ndiye Mungu umtumia.
Na ni kwa uhakika vile ulivyo vaa ni vile ulijiona kuwa ndio muonekano ambao wewe unapendeza na kujikubali ndio ulivyo hili nalo ni muhimu sana. Hivyo kweli nguo ni pambo basi jipambe vizuri ujiletee kujikubali mwenyewe na wengine.

Kama nguo haitoi ushuhuda wa kristo kwanini kujadiliwa?
-unafikiri kwanini nguo(mavazi) yamekuwa yakijadiliwa na kuwa tatizo miongoni mwa watu walio okoka na hata wasiookoka. Pamoja na hayo limekuwa sababu ya kanisa la Mungu kuchafuliwa na kupoteza umaana na heshima yake.
-hivyo tunajadili kuondoa  hilo tatizo na hatimae heshima ya mwili wa kristo pale Mungu alivyokusudia. Japo tunaenda na wakati ni vizuri kwenda nao pasipo kuwa kwazo kwa wengine.
Ni muhimu sana kama mkristo ujue huko uliko jamii yako inatakaje ili hao wakufurahie na waone uthamani wa uwepo wako.
Na ni vizuri kupata uelewa na ujue jinsi gani ya kuishi kwa akili katika jamii uliopo ukijitahidi ili usiwe kwazo.
“mwenye akili siku zote upenda kuona watu wanafurahia hata kama kwake ni maumivu kwake”
Fanya mazoezi kwa ajili ya wewe binafsi kuongeza marafiki  na kujiongezea uhuru wako.

Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                     Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com



“UKIJUA NI VIZURI KUMJULISHA”




                                                                                                                                         

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni