KUWA
MTUMISHI WA MUNGU
Kumtumikia Mungu Kama
apendavyo:
Ni jambo ambalo Mungu analitarajia
litokee kwa mtu ambaye amemkubali kuwa yeye ni Mungu wake.
Waefeso 4:1-4
Wafilipi 1:27-29
Kwa hakika maisha ya ushindi mwelekeo
sahihi wa kiMungu unakuja kwa usahihi ni pale tu utakapojua maana ya kumtumikia
Mungu, na hii ni kawaida ya Miungu yote haiwezi kukufanikisha mpaka pale
umeitumikia kwa namna inavyotaka yenyewe yani umewafanyia ibada ambayo
wamekubali.
Wakolosai 2:6
Hili neno la kawaaida masikioni mwa
watu wengi lakini kulisikia peke yake pasipo kueleweshwa na Mungu mwaenyewe ni
ngumu kulielewa kwa namna yake.
Ukitaka kuupendeza moyo wa Mungu lazima
ufikirie namna ya kufanya kitu mbele zake naye afurahie uwepo wako
duniani.(hiki ndicho Mungu anakitaka kwako maadam ukishakielewa hiki hakuna
kushindwa)
Na namna unavyomtumikia Mungu hicho
ndicho kipimo sahihi namna unavyo mpenda.(kutumika kwa kupenda ni vizuri kwakua
ni ishara ya kujua wajibu wako)
Kama kunakitu kikusumbue au kukinyime
raha ni kutafuta namna ya kumtumikia Mungu kwa usahihi wake pasipo
kushurutishwa wala kulazimishwa maana hapo ndipo palipo na ustawi wa maisha
yako yaani chemchem isiyokauka, raha yako itokane baada ya wewe kutambua maana
ya kumtumikia Mungu kuanza kumtukia Mungu.
Wafilipi 3:12
Sura ya Mungu,tabia zake,uwezo wake
utaona kwa ukamilifu pindi utakapo kuwa ndani ya utumishi wake.
Kitu cha maana kwa Mungu ni wewe
kuandaa mazingira ambayo Mungu atatenda kazi pamoja na wewe kwa namna yake.
Kama ukishindwa kutafuta na kujibidisha
namna ya kumtumikia Mungu sahau kuona
mtembeo wa ki Mungu ndani ya maisha yako na una haja kujivunia katika wokovu.
Iwathesalonike 1:8-9
Hii ni siri pekee ya kukaa na miungu
yoyote duniani ni kuitumikia na hakuna jambo linguine.
Nje
ya utumishi wa kweli mambo yote unayofanya hayana kibali kwa Mungu yaani
kutoa,kuomba,kuimba n.k
Na maisha haya ndiyo yanakupa nguvu
kusema mimi ni mali ya kristo kwa kuwa unamtukia yeye naye anayafurahia
muungamaniko wenu.
Kumtumikia Mungu sio shida si kwasababu
unaogopa jehanamu labda kuna urafiki kufanya jambo Kwa shirika lakini sio
kumtumikia Mungu Kama apendavyo yaani una mtumikia Mungu Kama alivyo hakuna
usaidizi mwingine.
.utendaji wa yesu ulitegemea Mungu
anasemaje?
Yohana 8:29
Hakuna kitu kigumu kama kumtumikia
Mungu katika matakwa yake yaani kufanya jambo kwa namna yake (vile awazavyo
katika akili yake Mungu)
I.hakuna kutoa hakuna kupata (no give no
gain)
Japo hatutoi ili kupata bali ni
kutekeleza maagano yetu kwake, ishara ya kuzingatia makubaliano yako na Mungu.
Maisha ni shamba japo si namna ya mwili
bali katika roho, kama hauta toa hakiwezi kupata
-shamba lina sifa kubwa kupanda na kuvunwa,
hivyo kama hakuna kupanda hakuna kuvuna hii ipo halisi sana.
Kutoa ni ishara kubwa sana kuwa Mungu
anahusika na maisha yako hivyo unahusika na mambo yake kwa kutoa KWA AJILI
YAKE.
Hili limekuwa jambo la adimu kwa watu
wanaoenda kanisani kwa sababu ya kutembea mwilini au kutoa maslai binafsi
kwanza.
Watu wengi hawaendi mbele kwa sababu
hawajajua misingi halisi ya kutoa,wanatoa pasipo ukamilisho.
Lazima ujifunze kutoa fedha,muda,nguvu
yako katika kuimarisha mwingiliano wako na Mungu. Utoaji wako mbele za Mungu
hiyo ni ishara kubwa ya kumtegemea Mungu
Utoaji uliokamili inamaana kuwa moyo
wako uko wazi kwa Mungu naye Mungu aweze kukupa kibali katika maisha yako.
Unapo penda kutoa muda wako,fedha na
vitu vingine havina shida nabado unaona haitoshi sikuzote utafikiri namna ya
kutoa zaidi ili akufurahie.
Usipotoa mwili wako kwa ajili Mungu
tambua utatumika kwa ajili ya mambo mengine,magonjwa,mawazo yasiyo kuwa na
maamuzi/yasiyo na muafaka wa kudumu na mambo mengi yatapata nafasi ndani
yako.(ndoto za kubomoa ufalme wa Mungu ndani yako,uvivu katika mambo ya Mungu)
Hii ni ishara ya kujipima kwa Mungu ni
namna gani unamjua,unamwitaji,thamni yako kwake hauhitaji kuweka mjadala
kujitambua.
Kwakua Mungu alionyesha kukupenda pale
tu alipotoa pumzi yake,uzima wake na hata mwanae wa pekee,kwaiyo utoaji ni
msingi mzuri kuonyesha upendo.
Yohana 3:16
Kuwa na kitu wakati unae mpenda
anakiitaji yupo hiyo si ishara ya kupenda hata kidogo(unayo nguvu,fedha n.k)
huo ni unafiki wa kiwango cha mbele za Mungu,haimfurahishi Mungu na muda si
mrefu utaona matunda ya kutomfurahisha Mungu(huwezi kutoka hatua moja kwenda
nyingine kiafya,kiuchumi).
Usipojitoa usitegemee yeye kujitoa
kwako.
Wagalatia 6:7
Prepared
by,
Cothey Nelson - 0764 018 535
cotheyn@yahoo.com
James katiti - 0713 398 042
james.adili19@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni