KIJANA WA MAANA:
Katika kuendelea juu ya kuwa kijana wa maana mbali
na kuwa na pesa tu na vitu vingi vinaonekana vya thamani kwa
mwanadamu.tunapenda tena tuangalie katika kipengele kinachofuata.
iii.uhuru na uamuzi
uliochukua
kila familia ina namna
ya kuchukulia au kulea watu wake katika jamii hiyo kuna watu waliokuwa na uhuru
na wengine waliokosa uhuru na wote kuna maamuzi waliochukua na hatimae wakawa
jinsi walivyo.
Hakuna jambo ambalo
linakaa katika moyo wako kwa muda mrefu kama maamuzi uliochukua halafu ukawekwa
katika hali mbaya, kwakua katika mazingira haya hakuna wa kulaumiwa ila ni wewe
binafsi.
Haijalishi ni
shindikizo gani lilikusukuma hatimae ukaamua maamuzi uliyo yachukua bali
kitakachoangaliwa hapo ni matokeo uliyo yachukua.
Yako maamuzi uliochukua
pasipo kujua kwa usahihi wa jambo husika na kuna maamuzi uliochukua kwakua
uliona ni sahihi kwa wakati ule lakini mwisho ukaujeruhi moyo wako.
Ezekieli
16:15-16,22-26
Unaweza ulipewa uhuru
mkubwa nyumbani kwenu kwa lengo la wazazi kutaka uyafurahie maisha yako na
uwafurahie wazazi wako lakini ukautumia ule uhuru katika maslahi yako pasipo
kuangalia usahihi wa kitu naam kasha ukaona matokeo yake.
Kumbuka kwamba jambo
ukisha lifanya linabaki kuwa historia katika maisha yako na wala haifutiki bali
inabaki kuwa kumbukumbu ambayo inaweza kuwa na nguvu ndani ya maisha yako au
isiwe na nguvu yote inakutegemea wewe binafsi.
Kunawezekana ulikuwa
unakataa kutokana na mafundisho mazuri uliyofundishwa na wazazi wako nay ale
uliyojifunza ukayafanya kuwa ni maisha yako lakini kutokana na maneno ya mtu
akakushawishi hatimae
ukaamua kukubaliana nae na hatimae ukaona matokeo yake
yanaweza kuwa mabaya au mazuri inategemea na jambao lenyewe.
Mathayo 7:10-23
Yamkini hapo awali
ulikuwa mtu mzuri sana hata wewe binafsi ulijitamani lakini ukakutana na rafiki
mbaye kwa kiasi kikubwa alibadilisha maisha yako na kuwa kwa namna ya yeye
ambayo ataifurahia (kutumia madawa ya kulevya(bangi,unga n.k), kujichua nawe
ukakubaliana na njia hizo kumbe unajiharibu kisakolojia(akili).hata Mungu
afurahi lakini kwa uhuru uliopewa ukaingia pengine hata bila ya kuruhusiwa
hatimae matokeo ukayaona.
II petro 2:14-15
Waefeso 5:11-12
HAKUNA RAFIKI ATAKAYE KUPENDA
KATIKA HALI YOTE,
(pendo la weza kupungua
hatimae kupotea kabisa. Yesu ndiye rafiki)
Yamuhimu:
I.rudi kwa
Mungu(wokovu)
Mungu anakupenda vile
ulivyo kwakua yeye ndie chimbuko la wanadamu lakini pindi utakapo okoka kwa
Mungu unakuwa na kibali kwa Mungu cha tofauti.
Hata kama umepoteza
mwelekeo jua kwamba ndani ya Mungu kuna mwelekeo sahihi ambayo ukimwamini basi
utapata mwelekeo sahihi.
Mungu si kama wanadamu
yeye afikiri kuhukumu bali ufikiria namna gani ya kukutoa mahali ulipo na kwenda
mahala pengine penye ubora wako katika maisha yako.
II nyakati
33:1-3,11-13
Ona ni kweli ulikuwa
unamtenda Mungu dhambi ya wazi au ya silini kiri kuwa wewe ndiye ambaye
ulimkosea Mungu na sasa umeamua kurudi kwa moyo wote pasipo kuangalia kushoto
wala kulia.
Mitahali 28:13
Onyesha ya kwamba
unamwitaji Mungu kuliko chochote kwakua ni ndani yake tu ndiko kuliko na
usalama na sio mahala pengine na ukijua lile alilopanga Mungu ndilo litakalo
timia na sio alilopanga mpenzi wako wala wewe binafsi kwa hiyo Mungu kiwa
upande wako kila kitu kitakuwa sawa.
Onyesha hali ya
kumwitaji Mungu kwakua yeye anaweza kubadilisha leo ikawa kesho na kesho ikawa
leo hivyo anauwezo wa kubadilisha historia yako akakupa historia nyingine iliyo
bora zaidi ya vile unavyofikiria.
Tambua ulitumia mwili
wako visivyo na wakati wako lakini sasa umeamua kutoa mwili wako kwa ajili ya
Mungu peke yake.
I wakorintho 6:19
II wakorintho 7:9-10
Prepared by ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
“Itakuwa vizuru tukikutana tena
katika wakati mwingine………..BARIKIWA”